Jeremiah 23:1-2

Tawi La Haki

1 a“Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asema Bwana. 2 bKwa hiyo hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema Bwana.
Copyright information for SwhKC